Friday, 24 March 2017
Rais Magufuli awataka wamiliki wa vyombo vya habari kuweka uzalendo mbele na kutotumia uhuru walionao vibaya
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John P. Magufuli, leo
amewaapisha Dr Harrison Mwakyembe na Prof Palamagamba Kabudi pamoja na
mabalozi kadhaa Ikulu Jijini Dar.
Mwakyembe ameapishwa kuwa Waziri mpya wa habari, Profesa Kabudi kaapishwa kaapishwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria.
==>Haya ni mambo machache aliyoyasema Rais Magufuli Leo
1.Kuna wengine walisema Kinana leo angezungumza na waandishi, wakati nimemtuma India ambapo atakuwa kwa zaidi ya siku 10
2.Tunataka kuitoa nchi katika hali ya mazoea kuipeleka katika mstari ambao ni sahihi
3.Ukiangalia siku iliyofuata baada ya Rais wa Benki ya Dunia kuja, magazeti yote yaliandika habari nyingine tofauti-
4.Niwatake waandishi wa habari muwe wazalendo, Tanzania ikiharibika na nyie pamoja na wanaowatuma muandike wote mtaharibikiwa
5.Hata magazeti ya leo yana picha ya mtu mmoja ambaye amefanya kosa moja, utadhani kosa ni linaungwa mkono na serikali
6.Niwatake wamiliki wa vyombo vya habari muwe waangalifu, kama mnadhani mna uhuru wa namna hiyo, kuweni makini sana
7.Kuna vyombo vingine vya habari sehemu yenye ugomvi ndio wanapeleka kamera na habari hizo zinapewa muda mrefu, 'watch out'
8.Vyombo vingine haviandiki mazuri ya mtu, lakini wakipata mabaya yake ndiyo yanajaza kurasa
Sunday, 19 March 2017
KMPDU wawakataa Madaktari wa Tanzania
Umoja
wa Madaktari, Wauguzi na Wataalamu wa Meno nchini Kenya ‘Kenya Medical
Practitioners, Pharmacists and Dentists’ Union’ (KMPDU) umepinga vikali
hatua ya Serikali ya Kenya kuleta madaktari kutoka Tanzania wakati Kenya
ina madaktari wengi ambao hawaajiriwa.
Kupitia
kwa Katibu Mkuu wa KMPDU, Ouma Oluga umepinga hatua hiyo na kudai kuwa
Serikali ya Kenya haijawa makini katika kushughulika na tatizo la
upungufu wa madaktari nchini humo.
Akizungumza na mtandao wa The Star wa nchini Kenya siku ya Jumamosi, Oluga alisema hata hivyo
watawakaribisha madaktari kutoka Tanzania na kuwaunganisha katika umoja
huo na kwamba watapaswa kupitia mitihani itakayoandaliwa na bodi ya
wauguzi.
Amesema mitihani hiyo itachukua sio chini ya miezi mitatu labda kama tu hitaji hilo halitaangaliwa.
“Kenya
ina zaidi ya madaktari 1,400 ambao wanasubiria ajira. Itakuwa gharama
kubwa na dalili ya kushindwa kutumia fedha za umma vizuri kwa kuwa na
madaktari 500 wa kitanzania kwa gharama ya Shilingi 20,000 kwa siku,” amesema.
Oluga
amesema kuwa Kenya inapaswa kupitia upya utaratibu wake wa Rasilimali
Watu kwa mujibu wa miongozo ya Afya kama ambavyo KMPDU imekuwa ikihitaji
hapo kabla.
“Hatuwezi kuwa tunafanyia majaribio maisha ya wakenya katika hali inayoonesha kutowajali wananchi,” ameongeza.
Mapema
jana Rais Magufuli alikubali na kuridhia ombi la Serikali ya Kenya na
kuahidi kutuma madaktari 500 kusaidia kukabiliana na tatizo la upungufu
wa madaktari nchini humo kufuatia mgomo wa madaktari ulioisha hivi
karibuni baada ya kudumu kwa siku 100
Saturday, 18 March 2017
LISSU ACHAGULIWA KUWA RAIS TLS
Wajumbe wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo wamefanya uchaguzi wa kumchagua rais pamoja na wajumbe wa ngazi mbalimbali za uongozi wa chama chao.
Uchaguzi huo umefanyika mjini Arusha ambako wanachama wa TLS wamekutana kutekeleza ratiba hiyo pamoja na kupanga mipango mbalimbali ya utendaji kazi wa chama hicho.
Matokeo ni kama ifuatavyo:
Urais: Kura zilizopigwa 1682
- Tundu Lissu 1411 sawa na asilimia 88
- Francis Stolla 64
- Victoria Mandari 176
- Godwin Mwapongo 64
==>Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais (TLS) mshindi ni Godwin Ngwilimi aliyekuwa Mwanasheria wa Tanesco na kutimuliwa kwa kupinga Escrow.
Council Members
- Jeremiah Motebesya
- Gida Lambaji
- Hussein Mtembwa
- Aisha Sinda
- Steven Axweso
- David Shilatu
- Daniel Bushele
#Habari:Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekubali kuipatia Kenya madaktari 500, watakaoisaidia nchi hiyo kukabiliana na tatizo la uhaba wa madaktari.
Serikali ya Kenya imesema ipo tayari kuwalipa stahili zote madaktari 500 watakaopatiwa kutoka Tanzania ikiwa ni pamoja na mishahara na nyumba za kuishi.
Friday, 17 March 2017
Video mpya ya super mafia
Subscribe to:
Posts (Atom)