Dallo Updaters Blog
Monday, 1 April 2019
Wednesday, 26 July 2017
Jinsi ya kuomba chuo mwaka huu 2017/2018
Habari yako?
Kwanza kabisa naepnda kumshukuru Mungu kwa kuzidi kunipa nguvu na akili ya kuzidi kuwatumia kwa kuwapa vitu muhimu hasa kipindi hiki cha uombaji wa vyuo vikuu 2017.
Watu wengi wamekuwa wakiuliza na kujiuliza je mwaka huu tunaombaje vyuo?
Maswayetu blog itaongelea jinsi ya kutuma maombi.
Kwa muda mrefu wanafunzi wengi wamekua wakiomba vyuo kupitia TCU au NACTE.Lakini mwa ka huu hali imebadilika ambapo wanafunzi watatakiwa kufanya application direct chuoni kupitia mfumo wa online ambao utakuwa umeandaliwa na chuo husika.
Lakini baadhi ya vyuo vinapokea maombi kwa njia ya barua ambapo hadi sasa hivi kuna vyuo 14 vilivyotoa form za kutuma maombi ya kujiunga masomo mwaka huu 2017/2018.
JINSI YA KUOMBA CHUO
Ili uweze kutuma maombi tafadhali ingia katika tovuti ya chuo husika ,kwa mfano unataka kwenda chuo kikuu SUA ,ingia google andika chuo kikuu SUA ,then itakuja official website ya SUA then ingia hapo,angalia habari mpya za admission ambazo ukiingia tu katika website husika lazima utakua Taarifa na form ya maombi.
ADA YA KUOMBA CHUO
Hapo awali watu walikua wanalipa tshs 50000 TCU na unaruhusiwa kuomba vyuo 5 unavyopenda kwenda,lakini kwa mwaka huu hali ipo tofauti kwani kila chuo utakachotaka kuomba lazima ulipie pesa,ambapo pesa ya maombi ina range kuanzia 20000 hadi 50000 inategemea na chuo,mfano endapo utataka kuomba vyuo 5 lazima uwe na kiasi kisichopungua 150,000/=.
KOZI NGAPI UNARUHUSIWA KUOMBA KWA KILA CHUO?
hii inategema na chuo husika kuna baadhi ya vyuo wanaruhusu kuomba hadi kozi tatu tofauti lakini kuna vyuo vingine unaruhusiwa kuomba kozi moja tu.
JE,USIPOCHAGULIWA CHUO ULICHOOMBA UNAFANYAJE?
Hili swala lipo hasa kutokana na competition,mfano Chuoni SUA kozi ya BVM inahitaji wanafunzi 70 tu,ambao waeomba ni wanafunzi 870,wakati wakufanya selection huwa wanaangalia mwanafunzi mwenye sifa za juu kushinda wote.
Basi endapo utaomba usipopata Chuo kinatakiwa kiwasilishe majina TCU ya wanafunzi waliokosa ili TCU watayatangaza nini cha kufanya.
Maombi yanataanza tarehe 22.7 2017 na kuishia one month later.
NOTE:kwa wanafunzi waliokosa sifa za kwenda chuo kikuu hadi sasa application zilishaanza na mwisho ni august 20 2017,kama unataka kuomba vyuo vya serikali tafadhali utaomba kupitia tovuti ya nacte.go.tz kwa afya na ualimu.
MWISHO
MASWAYETU BLOG INAKUTAKIA APPLICATION NJEMA NA TUNAOMBA ENDELEA KUTEMBELEA BLOG YETU KWA HABARI ZAIDI KUHUSU VYUO VILIVYOANZA KUPOKEA MAOMBI
Majina ya vyuo 19 vilivyozuiwa na TCU kuandikisha wanafunzi mwaka 2017/18 na Kozi zilizofungiwa
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa imefanya uhakiki wa vyuo vyote vya elimu ya juu nchini ili kuhakiki ubora wa elimu inayotolewa vyuoni hapo, ripoti ya uhakiki huo ilionyesha mapungufu kadhaa katika baadhi vyuo.
Hivyo tume imeamua kuchukua uamuzi wa kusitisha udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18 kwa vyuo hivyo.
Aidha, Tume hiyo imevitaja vyuo hivyo kuwa ni pamoja na:
- Eckenforde Tanga University
- Jomo Kenyatta University, Arusha
- Kenyatta University, Arusha
- United African University of Tanzania
- International Medical and Technological University (IMTU)
- University of Bagamoyo
- Francis University College of Health and Allied Sciences
- Archibishop James University College
- Archibishop Mihayo University College
- Cardinal Rugambwa Memorial University College
- Kampala International University Dsm College
- Marian University College
- Johns University of Tanzania Msalato Centre
- Johns University of Tanzania, Marks Centre
- Joseph University College of Engineering and Technology
- Teofilo Kisanji University
- Teofilo Kisanji University Tabora Centre
- Tumaini University, Mbeya Centre
- Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMCo)
Aidha, kutokana na mapungufu hayo katika vyuo mbalimbali imeamriwa kuwa jumla ya programu 75 kutoka vyuo 22 nchini zimesitishwa kudahili wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/18.
Programu ambazo zimesitishwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/18 ni pamoja na
Baada ya Msiba wa Mkewe......Mwakyembe Leo Kaongea na Waandishi wa Habari
Leo Jumatano ya July 26 ikiwa ni siku 11 zimepita toka utokee msimba wa mke wa waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Dr Harrison Mwakyembe, leo ameongea na vyombo vya habari nyumbani kwake Kunduchi Dar es Salaam.
Mwakyembe amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kuombeleza kifo cha mkewe Linah Mwakyembe kilichotokea usiku wa Julai 15 mwaka huu kwenye Hospitali ya Aga Khan.
Dk Mwakyembe pia amemshukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa mchango mkubwa walioutoa katika kumuuguza mkewe
Saturday, 24 June 2017
Thursday, 15 June 2017
Friday, 9 June 2017
NEW. POSTS ZA FORM FIVE ZIMETOKA
Subscribe to:
Posts (Atom)